Biashara ya Nguo za Mitumba

Ujasiriamali

by Ali Mwambola

Product Description:

Kitabu hiki kimetayarishwa kutokana na mwitikio mkubwa niliopata, kutoka kwa wadau, walio ona video yangu inayoitwa 'Jinsi ya kuanzisha biashara ya nguo za mitumba' ambayo inapatikana kwenye You Tube Channel ya Ali Mwambola

 

Nimekuwa nikipata simu pamoja na SMS messages nyingi kutoka kwa wadau ambao wamekumbana na chanagamoto mbali mbali, wakati wakiwa katika mipango ya kuanzisha biashara ya nguo za mitumba

 

Kuna baadhi ya wajasiriamali wanadhani kuwa, unapokuwa unao mtaji wa kutosha, basi unaweza kuanzisha biashara ya nguo za mitumba na kupata mafanikio.

 

Hayo ni mawazo yanayo potosha, kwa kuwa kuna taratibu ambazo zinatakiwa utekeleze ili mafanikio yapatikane

Hiki kitabu kinaeleza taratibu za kutekeleza, ili ufanikiwe kuanzisha biashara ya nguo za mitumba yenye mafanikio.