Mfumo wa Kuendesha Biashara
Ujasiriamali
by Ali Mwambola
Kuna tatizo la biashara nyingi kuanzishwa bila ya kuweka malengo ya biashara ambayo imeanzishwa
Hali hii, husababisha biashara nyingi kuendeshawa mfano wa gari ambayo imekosa mwelekeo. Kwa kawaida, biashara inayo endeshwa bila ya kuwa na malengo, hatima yake huwa sio nzuri
Mara nyingi, biashara inayo kosa malengo, hatima yake huwa kufilisika ndani ya muda mfupi, tangu kuanzishwa
Unapo anzisha biashara bila ya kuweka malengo, hali hii husababisha kukosekana hamasa ya kupata mafanikio
Kukosekana hamasa ya kutaka kupata mafanikio, husabisha kukosekana mipango, mbinu, mikakati ya kufanikiwa katika biashara
Usikubali kufanya biashara bila ya kuwa na malengo, hivyo kusababisha changamoto nyingi. Unapotaka kuanzisha biashara, kuna mambo mengi muhimu unatakiwa utekeleze
Huwezi kutekeleza mambo yote kwa ufanisi, kama hauna malengo, ambayo yatakupa msukumo wa kutekeleza mambo mengi muhimu
Njia fupi ya kufanikiwa kufikia malengo ya biashara, ni kutumia mfumo mzuri wa kusimamia biashara
Kitabu hiki kinaeleza jinsi ya kuweka mfumo mzuri wa biashara, ambao unafakisha kufikia malengo ya biashara yaliyowekwa