Kuanzisha Biashara ya Stationery
Ujasiriamali, #7
by Ali Mwambola
Moja kati ya biashara ambayo imekuwa inavutia wajasiriamali ni biashara ya stationery
Wapo wajasiriamali ambao wamefanikiwa kuanzisha biashara za stationery, ambazo zinapata faida na hivyo kuwa endelevu
Kuna wengine hawajafanikiwa kuwa na biashara ya stationery, ambazo zinapata faida na hivyo kuwa endelevu
Kufanikiwa kuwa na biashara ya stationery ambayo ni endelevu, hutegemea kama biashara imeanzishwa kwa kufuata taratibu zinazo kubalika
Baadhi ya wajasiriamali hudhani kuwa, unapokuwa na mtaji wa kutosha kuanzisha biashara, basi unaweza kuanzisha biashara ya stationery ambayo itakuwa endelevu
Hayo mawazo sio sahihi, kwani usipo tekeleza taratibu zinazo kubalika za kuanzisha na kuendeleza biashara, ni dhahiri kuwa, hiyo biashara itayumba au kufilisika kabisa
Hiki kitabu kinaeleza taratibu za kutekeleza, ili ufanikiwe kuanzisha biashara ya Stationery yenye mafanikio.