Biashara ya Vinywaji
Ujasiriamali
by Ali Mwambola
Moja kati ya biashara ambayo imekuwa inavutia wajasiriamali ni biashara ya vinywaji
Wapo wajasiriamali ambao wamefanikiwa kuanzisha biashara ya vinywaji ambayo inapata faida na hivyo kuwa endelevu
Kuna wengine hawajafanikiwa kuwa na biashara ya vinywaji ambayo inapata faida na hivyo kuwa endelevu
Kufanikiwa kuwa na biashara ya vinywaji ambayo ni endelevu hutegemea kama biashara imeanzishwa kwa kufuata taratibu zinazo kubalika
Baadhi ya wajasiriamali hudhani, unapokuwa na mtaji wa kutosha kuanzisha biashara, basi unaweza kuanzisha biashara yeyote ambayo itakuwa endelevu
Hayo mawazo sio sahihi, kwani usipotekeleza taratibu zinazo kubalika za kuanzisha na kuendeleza biashara, ni dhahiri kuwa hiyo biashara itayumba au kufilisika kabisa
Hiki kitabu kinaeleza taratibu za kutekeleza, ili ufanikiwe kuanzisha biashara ya vinywaji ambayo ni endelevu