Jinsi ya kuanzisha biashara mpya ya duka
Ujasiriamali
by Ali Mwambola
Kuna baadhi ya wajasiriamali wanadhani kuwa, unapokuwa na mtaji wa kutosha, basi unaweza kuanzisha biashara ya duka, na kupata mafanikio
Hayo ni mawazo yanayo potosha, kwa kuwa kuna taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa ili mafanikio yapatikane
Hiki kitabu kinaeleza taratibu za kufuata, ili mjasiriamali afanikiwe kuanzisha biashara ya duka yenye mafanikio
Jambo la msingi ni kwa mjasiriamali kuhakikisha kuwa hapo anapotaka kuanzisha duka, kuna uwezekano mkubwa wa kupata wateja. Kwa sababu kama hakuna wateja, basi hakuna biashara.
Mjasiriamali anapokuwa na uhakika wa kupata wateja wa duka analotaka kufungua, basi anaweza kushughulikia taratibu nyingine zinazo pendekezwa za uanzishaji wa biashara ya duka
Ni matumaini yangu kuwa, ukimaliza kusoma hiki kitabu, utakuwa umepata elimu ya kutosha, kuhusu hatua ambazo mjasiriamali anatakiwa kuchukua anapotaka kuanzisha biashara ya duka