Uanzishaji biashara ya salon

Ujasiriamali

by Ali Mwambola

Product Description:

Unapotaka kuanzisha biashara ya salon ni muhimu ufahamu kuwa kuna mambo muhimu inabidi utekeleze kama unataka kumiliki salon yenye mafanikio

Siku zote biashara huanzishwa pale mjasiriamali anapoona changamoto wanazokabiliana wateja na kuzigeuza hizo changamoto kuwa fursa

Fursa za kufanya biashara ya salon zinatona na changamoto wanazokuwa nazo wateja zinazohusu mahitaji yao ya kila siku ya huduma za salon.

Kwa hiyo wajibu wa mjasiriamali ni kutambua hizo changamoto za wateja na kuzigeuza kuwa fursa za kufanya biashara ya salon

Ili upate msukumo wa kutumia fursa zinazo jitokeza ni muhimu uwe na dhamira ya kufanya biashara ya salon.

Dhamira yako inabidi itekeleze mambo yanayuhusu soko la wateja wa salon na mahitaji ya wateja ndani ya soko la biashara ya salon

Kitabu hiki kimeeleza mambo yote muhimu ya kutekeleza wakati una anzisha biashara ya salon

Ni matumaini yangu kuwa, ukimaliza kusoma hiki kitabu, utakuwa umepata mwanga, kuhusu hatua za kuchukua, unapotaka kuanzisha biashara ya salon