Tengeneza Hesabu za Biashara
by Ali Mwambola
Hiki kitabu kimechapishwa kuwasaidia wajasiriamali ambao hawana elimu ya uhasibu
Sasa hivi ninafanya kazi kama Business Consultant, ninayetoa ushauri kwa wajasiriamali na wafanyabiashara mbali mbali
Nimejaribu kuwauliza wafanyabiashara wengi na wajasiriamali, kama biashara zao zinapata faida au hasara
Nimesikitika baada ya kufahamu kuwa wengi wao, hawafahamu kama wanapata faida au hasara, kwa sababu hawatengenezi hesabu za biashara zao
Sababu wanayotoa ya kutotengeneza hesabu za biashara zao, ni kuwa, hawana uwezo wa kifedha wa kuajiri wahasibu
Kutokana na hali hiyo, nimeamua kusaidia kupata ufumbuzi wa hili jambo, kwa kuchapisha hiki kitabu
Nimeandika hiki kitabu kwa kutumia lugha nyepesi ya kihasibu, kusudi nieleweke na wengi ambao hawana elimu ya uhasibu
Majarajio yangu ni kuwa, nitakuwa nimewasaidia wajasiriamali wengi kuweza kutengeneza hesabu za biashara zao wenyewe