Biashara ya Duka la Nguo
Ujasiriamali, #5
by Ali Mwambola
Unapotaka kuanzisha biashara ya nguo ni muhimu ufahamu kuwa kuna mambo muhimu inabidi utekeleze kama unataka kumiliki duka la nguo lenye mafanikio
Jambo la msingi kuelewa ni kuwa usianzishe biashara ya duka la nguo kwa kuwa jirani yako, ndugu yako au rafiki yako anamiliki duka la nguo lenye mafanikio
Hakikisha kwanza kuwa biashara ya duka la nguo imekuwa mawazoni mwako muda mrefu kwa kuwa unaipenda. Lazima uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuanzisha hii biashara, sio kwa sababu umeona mtu mwengine amefanikiwa katika biashara ya nguo
Mjasiriamali unaweza kuanzisha biashara ya duka la nguo baada ya kujiridhisha kuwa eneo fulani kuna wateja ambao wanakabiliana na changamoto mbali mbali zinazohusiana na biashara ya nguo. Hivyo unachofanya ni kuzigeuza hizo changamoto za hao wateja, kuwa fursa ya kufanya biashara ya duka la nguo.
Kwa hiyo wajibu wa mjasiriamali ni kutambua changamoto za wateja wa biashara ya nguo na kuzigeuza kuwa fursa za kufanya biashara
Ali Mwambola
Dar es Salaam