Utengenezaji wa Business Plan

Ujasiriamali

by Ali Mwambola

Product Description:

Unapotaka kuanzisha biashara, kuna mambo mengi muhimu unatakiwa utekeleze

Huwezi kutekeleza mambo yote kwa ufanisi kama hauna maandiko yatakayo kuongoza.

Unatakiwa uwe na Business Plan, ambayo ni dira itakayo kuongoza kuanzisha na kusimamia biashara yako

Business Plan nzuri, ni ile inayo kuongoza kuanzia mwanzo hadi pale utakapo anzisha biashara yako mpya

Business Plan, pia inaweza kukusaidia kupata mkopo, kutoka benki na fedha kutoka kwa wawekezaji au wahisani, kwa ajili ya biashara

Wanaotoa fedha, huwa wanahitaji kuhakikishiwa kuwa, fedha yao kuna uwezakano wa  kurudishwa

Kabla hujatengeneza business plan ya biashara, ni muhimu kwanza ujiridhishe kuwa, kuna fursa ya kufanya biashara unayotaka kuanzisha

Natumai ukimaliza kusoma hiki kitabu, utafahamu hatua za kuchukua unapo tengeneza Business Plan ya biashara yako