Kuanzisha Biashara Endelevu
Ujasiriamali
by Ali Mwambola
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru walio saidia kufanikisha uchapishaji wa hiki kitabu. Kitabu hiki kimetayarishwa kutokana na mwitikio mkubwa niliopata, kutoka kwa wadau, walio ona video yangu inayoitwa 'Jinsi ya kuanzisha biashara mpya"
Video inapatikana kwenye You Tube Channel www.youtube.com/alimwambola
Nimekuwa nikipata simu pamoja na SMS messages nyingi kutoka kwa wadau ambao wamekumbana na chanagamoto mbali mbali, wakati wakiwa katika harakati za kuanzisha biashara mpya
Kuna baadhi ya wajasiriamali wanadhani kuwa, unapokuwa unao mtaji wa kutosha, basi unaweza kuanzisha biashara na kupata mafanikio. Hayo ni mawazo yanayo potosha, kwa kuwa kuna taratibu ambazo zinatakiwa kufuata ili mafanikio yapatikane
Hiki kitabu kinaeleza taratibu za kufuata, ili ufanikiwe kuanzisha biashara yenye mafanikio.