Mtaji wa Kuanzisha Biashara
Ujasiriamali
by Ali Mwambola
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru walio saidia kufanikisha uchapishaji wa hiki kitabu. Kitabu hiki kimetayarishwa kutokana na maswali mengi ambayo nimekuwa napata kutoka kwa wajasiriamali kuhusu mtaji wa kuanzisha biashara
Wajasiriamali wengi wanadhani kuwa kuna kiasi maalum cha fedha ambacho kinatosha kuanzisha biashara za aina mbali mbali
Mfano wa maswali ambayo nimekuwa napata ni kama ifuatavyo:
"Kiasi gani cha mtaji kinatosha kuanzisha biashara ya stationery"
"Mimi ninazo shs 1,500,000 ambazo ninataka nianzishe salon, naomba ushauri iwapo hizo fedha zinatosha"
"Naomba ushauri jinsi ya kupata mtaji kutoka bank wa kuanzisha garage ya magari"
"Shilingi ngapi zinatosha kuanzisha biashara ya unga wa sembe?"
Ukweli wa mambo ni kuwa, hakuna kiasi maalum cha fedha ambacho kinaweza kutumika kama mtaji wa kuanzisha biashara
Mjasiriamali mmoja anaweza kuanzisha duka la vipodozi kwa shs 5,000,000 na mwengine anaweza kutumia shs 50,000,000 kuanzisha biashara ya vipodozi
Unachotakiwa kufahamu ni kuwa, kuna vigezo maalum ambavyo hutumika wakati wa kukadiria ukubwa wa mtaji ambao una tosha kuanzisha biashara
Hiki kitabu kinaeleza mambo mbali mbali muhimu kuhusu mtaji wa biashara pamoja na maelezo ya jinsi ya kukadiria mtaji wa biashara na wapi unaweza kupata fedha za mtaji
Ali Mwambola
Dar es Salaam